Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Mchemba ameagiza vyombo vya ulinzi Nchini kuwatumia Wafungwa wenye taaluma katika kazi za maendeleo na uzalishaji kwani ni bora kwa wafungwa wenye tabia njema na wale ambao wamejirekebisha tuwatumie kuwapa kazi kwa mikataba kuliko kuwarudisha uraiani ambako watakuwa hawana mitaji mwishowe wanaweza wakarudia na tabia chafu zilizo waweka Jela. Mwigulu ameongea hayo katika Ufunguzi wa Nyumba tano Mkoani Arusha ambazo zimejengwa na Askari Magereza kushirikiana na Wafungwa Waziri amesema kupitia Jeshi la Magereza watakujengea Nyumba kwa bei ndogo tofauti na kuchukuwa Mainjinia wa nje ya Magereza.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.