August 02, 2016

SIMBA SPORT CLUB IMEPOTEA AU IMEPATIA KWA MO' DEWJI?

MO" Unaweza kumuita hivyo nikijana wa kitanzania mwenye asili ya India alizaliwa mkoani Singida nakulelewa na wazazi wake mkoani hapa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi Serikalini ikiwemo Ubunge katika jimbo moja hapa singida

MO" ni bilionea kijana namba moja Africa na nitajiri namba 7 Africa watuwengi wamekuwa wakijiuliza sana juu ya utajiri wake kwani amekuwa na utajiri ambao wa Tanzania hawakutegemea nafasi hii kushikwa na kijana mdogo kama huyu nakuweza kuwabwaga wenzake Bakharesa Mengi, Manji,
 Ndesamburo, na wengine wengi lakini tumeshuhudia katika serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais mchapa kazi John Pombe Magufuli inayo sisitiza kulipa kodi

Hivi karibuni tumeshuhudia matajiri wa kubwa hapa Nchini wakibainika kuiibia serikali kwa kuto kulipa kodi baadhi ya watu walitegemea kuona kunagundulika ufisadi mkubwa wakuiibia mapato Serikali kutoka kwa tajiri huyo hakika usilolijuwa sawa na usiku wa giza hakika utajiri wake umekuwa na faida kubwa kwa serikali kwani amekuwa  mlipaji kodi mzuri kwa Serikali

AITAKA SIMBA  ni stori ambazo zilikuwa zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii takribani wiki moja sasa  jumapili ya tarehe 31/7/2016 kulifanyika mkutano mkuu wa mwaka wa club ya Simba uliolenga kupitia maendeleo ya club na kujuwa mapato na matumizi kwa mwaka ya club lakini ilipofika kwenye ajenda namba 9 hapo ndipo palimuhusu sana mo" kwani biliponea huyu alitoa tamko kwamba anataka awekeze katika club hiyo wana msimbazi kwa hisa ya asilimia 51% pia mo" alitoa ufafanuzi kuwa atawekeza kiasi cha tsh.bilioni 20 katika club hiyo idadi yawanachama waliohudhuria mkutano huo ni zaidi ya watu 300 na wote walipenda timu yao iendeshwe kwa mtindo wa uwekezaji


Mo" alikuwa yupo nyumbani kwake akiwatuma wanausalama wake wafuatilie mkutano huo lakini kwake alisubiri jambo moja tu kwa wa nachama ndio amwage cheche zake hakika wanachama wa simba wamechoshwa nakuitwa wa matopeni hasa watani wao wa jadi YANGA mkutano uliisha kwa makubaliano ya wanachama kutaka MABADILIKO ndani ya club hiyo Rais wa club ya simba Evance Aveva amekubali mabadiliko hayo yalio pitishwa na wanachama sasa matumaini ya wana simba yameanza kurudi baada hapo jana MO" kutamka kuwa hata usajili unaoendelea viongozi wasimba waende ofisini kwake wakachukuwe mkwanja wanaouhitaji kwa kumalizia usajili uliobakia swali ni hili SIMBA SPORT CLUB IMEPOTEA AU IMEPATIA KWA MO" DEWJI?

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.