Abiria mmoja aliekuwa akifanya safari yake kutoka Dar es salaam kwenda Jijini Tanga amejikuta akifupisha safari yake baada ya kuona kijiwe cha kuuzia Pweza umbali wa kilomita 2 tu kabla ya kuingia Tanga.Abiria huyo ambae bado jina lake halikuweza kufahamika mara moja alisikika akimwambia konda konda konda, mwenge hauvuki kijiji niache hapo kondakta akamjibu hutushushi hapa hapana kituo abiria akamwambia nisaidie nimeshafika bana abiria wote kwenye gari wakamuunga mkono mshushe tu amefika kwao.Baada ya kushuka akaelekea kando kidogo kwenye banda la kuuzia Pweza akapaza sauti hii kitu ni adimu sana wacha nipige nitakuja hata kwa boda boda abiria wote wakaangua vicheko
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.