Mwimbaji wa Injili Rehema kaparata awapa taarifa hii mashabiki zake kwa mwaka huu wa 2018. Akipiga stori na mtu mweusi gospel amesema ndani ya mwaka huu anatarajia kuachia project yake mpya, aah mwaka huu natarajia kuwa na project ila sitaki kuiweka wazi ni mwezi gani lakini ndani ya mwaka huu.
Alipoulizwa juu ya kuwa na album amesema mipango ipo japo kunakuwa nachagamoto mbali mbali ikiwemo kupata promo unajuwa ndugu mwandishi unaweza ukafanya album ukajikuta unakosa promo mwishowe unakuwa upo kwenye hasara.
Waimbaji wengi wa Injili hatupati sapoti kubwa katika kupromot nyimbo zetu hasa ukiwa mchanga jnabakia kufanya matamasha ya ndani.Kunawakati natamani labda kazi yangu nipeleke studio kuitambulisha gharama unazoambiwa unashindwa kuzimudu.
Mtu mweusi gospel
Nini maoni yako
Rehema kaparata
Vyombo husika viwe vinatupa nafasi ya kutambulisha nyimbo zetu kwani aslimia kubwa wasanii wa dogo hatuna uwezo wa kipato ambacho Media wanaitaji.Hizi kazi tunafanya kwa hasara ukizingatia tunafanya kazi kwakujitoa kama unaombwa kwenda kuhudumu mkutanoni kunawakati unakosa nauli ya kwenda kutoa huduma ya uimbaji mikutanoni.
Mwisho Mungu awabariki Media zote
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.